Dagaa

From Wikipedia, the free encyclopedia

Dagaa
Remove ads

Dagaa ni jina la kawaida la samaki wa oda Clupeiformes isipokuwa spishi za familia Chirocentridae. Spishi nyingi zina majina mengine pia, kama vile kapenta, kerenge, lumbu, mbarata, mwatiko, ndakala, pata, pawali, simu, uono na usipa. Spishi kadhaa za familia Alestidae, Apogonidae, Atherinidae, Cyprinidae na Leiognathidae huitwa dagaa pia lakini majina mengine yanapendelewa.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...

Dagaa wanatokea katika bahari zote za dunia na katika maziwa na mito mingi. Aina ambayo hupatikana tu katika Ziwa Tanganyika ni:

  • Limnothrissa miodon
  • Stolothrissa tanganicae

Kibofuhewa cha Clupeiformes kimeungana na utumbo kwa kifereji. Kwa kawaida hawana mrabafahamu (mstari wa ubavu, lateral line kwa Kiingereza) lakini wana macho, mapezi na magamba ambayo ni ya kawaida kwa samaki wengi, ingawa siyo samaki wote wana sifa hizi. Wao ni samaki wenye rangi ya fedha na mwili mwembamba wenye umbo la dulabu, na mara nyingi huunda makundi. Takriban spishi zote hula planktoni ambazo huzichuja kutoka kwa maji kwa matamvua yao.

Remove ads

Spishi zilizochaguliwa za Afrika ya Mashariki

Remove ads

Picha

Marejeo

  • Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
  • Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.

Viungo vya nje

Dagaa kwenye hifadhidata ya samaki Ilihifadhiwa 13 Agosti 2019 kwenye Wayback Machine.

Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dagaa kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads