Dawa ya famasia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Dawa ya famasia (kwa Kiingereza pharmaceutical, medicament au drug) ni dawa inayotumika kwa upimaji, tiba na kinga ya maradhi.[1][2][3]

Namna ya kutumia dawa (kwa Kiingereza pharmacotherapy) ni sehemu muhimu ya uganga wa kisayansi na inategemea fani ya utengenezaji wa dawa (pharmacology) kwa ajili ya ustawi wa mfululizo na inategemea ufamasia kwa matumizi ya kufaa.
Dawa hizo zinaainishwa namna mbalimbali, kama vile kulingana na mtaalamu gani anaweza kuziagiza kwa mgonjwa, au kulingana na asili ya dawa, au kulingana na lengo la tiba. Shirika la Afya Duniani lina orodha ya dawa muhimu zinazotarajiwa kupatikana kokote.
Utengenezaji wa dawa unahitaji kazi na gharama kubwa ambazo kwa kawaida ni juu ya wanasayansi na kampuni za kifamasia. Kwa kawaida serikali inaratibu biashara ya dawa.
Remove ads
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads