Desibeli

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Desibel (kutoka Kiingereza: decibel; kifupi: dB) ni kizio cha upimaji wa nguvu au ukali. Kinalinganisha vipimo viwili kwa kutumia logi.

Matumizi yake ni hasa katika upimaji wa sauti na katika teknolojia ya umeme kwa kutaja kuongezeka au kupungua kwa volteji au sauti.

Kizio cha msingi ni "bel" na desibel ni sehemu yake ya kumi.

Nyongeza ya desibeli 3 inalingana takriban na kuzidisha nguvu mara mbili.

Kizio cha msingi cha bel kilipata jina lake kwa kumbukumbu ya Alexander Graham Bell aliyekuwa mmoja wa wabunifu wa simu.

Mara nyingi, desibeli hutumiwa kutaja ukubwa wa sauti kulingana na jinsi tunavyoisikia.

Decibel si kipimo sanifu cha SI.

Baadhi ya mifano ya sauti ni:

Maelezo zaidi Kiwango cha Sauti, Mifano ...
Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads