Simu

kifaa cha mawasiliano ya simu From Wikipedia, the free encyclopedia

Simu
Remove ads

Simu (kutoka Kiarabu سیم, sim, inayomaanisha "waya") ni kifaa cha elektroniki kinachotumika kwa mawasiliano ya mbali kwa kutumia sauti, ujumbe wa maandishi, au njia nyingine za kidijitali.

Thumb
Simu ya mezani
Thumb
Simu za mikononi
Thumb
Simujanja

Ina uwezo wa kupokea na kutuma taarifa sehemu mbalimbali kupitia mtandao wa mawasiliano, kama vile simu za mkononi au simu za mezani. Simu pia inaweza kuwa na huduma nyingine kama kamera, kumbukumbu, na uwezo wa kupata mtandao wa intaneti, na hutumika kwa madhumuni mengi kama vile mawasiliano ya binafsi, kazi, au burudani.

Awali simu ilihitaji iunganishwe na nyaya, lakini leo hii inaweza kutumia redio. Hiyo inaitwa nyayatupu, siwaya au simu bila waya.

Remove ads

Historia

Watu wengi wanaamini kuwa simu iligunduliwa mnamo 1876 na Alexander Graham Bell,[1] Mskoti mwenye umri wa miaka 29 aliyeishi nchini Marekani. Lakini Mwitalia Antonio Meucci alianzisha matumizi ya simu toka mwaka wa 1871 hukohuko Marekani.

Tangu mwishoni mwa karne ya 20 kuna aina mpya ya simu iliyoenea ambayo ni simu za mikononi. Ingawa haistahili kweli kuitwa tena "simu" kwa maana asilia kwa sababu hakuna simu, ni aina ya mtambo wa mawasiliano uliosambaa haraka sana.

Katika nchi nyingi za Afrika simu hizi zina faida ya pekee kwa sababu zinaruhusu mawasiliano hata pale ambako nyaya za Posta hazifiki.

Remove ads

Namba za simu

Kila simu inapaswa kuwa na namba ya pekee ikiunganishwa katika mtandao wa simu. Isipokuwa ofisi au kampuni inaweza kuwa na namba moja kwa simu zake zote halafu maungio ya simu ya ndani ambako ama mtu au mtambo unaunganisha simu za ndani na mtandao wa nje.

Kwa kawaida mtandao wa simu ndani ya nchi inagawiwa kwa maeneo. Maeneo haya yanaweza kugawiwa tena hadi ngazi ya mtandao wa mahali. Kila eneo linafikiwa kupitia namba ya eneo; ndani ya eneo inatosha kutumia namba ya simu yenyewe.

Mfano: simu ya namba 556677 iko mjini Dar es Salaam. Namba ya eneo la Dar es Salaam ni 022. Kufikia simu hii ndani ya eneo la Dar es Salaam inatosha kupiga 556677. Mtu anayetaka kuipigia kutoka Dodoma au Arusha anatangulia namba ya eneo na kupiga 022-556677.

Simu za mkononi huunganishwa katika mtandao mkubwa wa kitaifa kufuatana na kampuni inayotoa huduma kama vile Airtel, TIGO au TTC yenye mtandao wake wa pekee. Kwa teknolojia bila waya hakuna haja ya ugawaji wa kieneo. Lakini kwenye simu hizi ni lazima kutumia pia namba ya mtandao muda wote. Kwa kupiga simu ya kawaida kutoka simu ya mkononi ni lazima kutumia muda wote namba ya kieneo hata kama mwenye kupiga yuko mji uleule maana mitandao ni tofauti.

Remove ads

Tazama pia

Marejeo

Loading content...

Viungo vya nje

Loading content...
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads