Fugo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Fugo
Remove ads

Fugo (ing. domestication kutoka lat. domesticus: "kuhusiana na nyumba") ni mchakato unaotoeka kama wanyama mwitu wanaishi karibu na watu na kufugwa nao kwa muda mrefu.

Thumb
Mbwa kaya anaaminiwa kuwa mnyama wa kwanza aliyetokwakwa njia ya fugo
Thumb
Mbwa mwitu wa Ulaya alikuwa babu wa mbwa kaya

Uteuzi wa tabia za wanyama

Katika muda wa vizazi vingi tabia mbalimbali za wanayama zinabadilika. Hii inatokea hasa kwa sababu watu waliteua wanyama wenye tabia zilizotakiwa, kwa mfano

  • ukali ya kupungukiwa
  • uvumulivu kwa kukaa karibu na binadamu
  • kiasi cha nyama au maziwa au sufu
  • uwezo wa kutumia chakula kilicholiwa na binadamu
  • idadi ya watoto na uwingi wa kuzaa

Katika mchakato wa uteuzi wanyama wasiolingana hawakupewa nafasi ya kuzaa tena yaani hawakufugwa na hivyo tabia zisizotakiwa zilipugua na tabia zilizotafutwa ziliongezeka.

Remove ads

Fugo kwa mimea

Mchakato huohuo ulitokea pia upande wa mimea.

Watu walikuta manyasi yenye mbegu kubwa kiasi uliofaa kama chakula wakatambua ya kwamba waliweza kutunza mbegu za aina hii ya nyasi na kuzipanda mahali walipohamia wakaona wakitunza mbegu kubwa zaidi kwa kupanda polepole mimea mpya ikaota mbegu kubwa zaidi.

Katika mchakato huu kipo chanzo cha kutokea kwa nafaka zote zinazoliwa na binadamu. lakini pia mimea mingine ya matunda kama vile ndizi au mitofaa.


Remove ads

Kujisomea

  • Charles Darwin, The Variation of Animals and Plants under Domestication, 1868.
  • Jared Diamond, Guns, germs and steel. A short history of everybody for the last 13,000 years, 1997.
  • Laura Hobgood-Oster, A Dog's History of the World: Canines and the Domestication of Humans, 2014
  • Hope Ryden, Out of the Wild: The Story of Domesticated Animals Hardcover, 1995
  • Halcrow, S. E., Harris, N. J., Tayles, N., Ikehara-Quebral, R. and Pietrusewsky, M. (2013), From the mouths of babes: Dental caries in infants and children and the intensification of agriculture in mainland Southeast Asia. Am. J. Phys. Anthropol., 150: 409–420. doi: 10.1002/ajpa.22215
  • Hayden, B. (2003). Were luxury foods the first domesticates? Ethnoarchaeological perspectives from Southeast Asia. World Archaeology, 34(3), 458-469.


Viungo vya Nje

Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads