Dura ya maji
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Dura ya maji (en:water cycle) ni jinsi gani maji huzunguka duniani kuanzia uso wa ardhi, angani hadi uso wa ardhi tena na chini ya ardhi. Maji huzunguka kwa kutumia michakato wa uvukizaji na usimbishaji.

Dura
- Kwanza maji yaliyopo kwenye uso wa ardhi huvukiza. Maana yake miale ya jua inapashia joto maji kwenye nchi kavu au baharini na maji hayo hubadilika kuwa mvuke ambao ni mwepesi na kupanda juu kwenye angahewa.
- Mvuke wa maji unaingia katika akiba kubwa ya maji kwenye angahewa; kutegemeana na halijoto ya hewa maji hukaa huko kama gesi au yanaendelea kujikaza kuwa mawingu.
- Wakati mawingu hupoa zaidi mvuke unaendelea kujikaza na kutonyesha.
- Hapa usimbishaji unaanza na maji huanguka chini kwa umbo la mvua au theluji.
- Mvua hugonga uso wa ardhi. Sehemu inapita juu ya uso wa ardhi kwenye mito moja kwa moja. Sehemu nyingine inaingia katika udongo wa ardhi. Kutoka hapo italisha chemchemi.
- Kutoka chemchemi maji hutokea kwa umbo la mito na vijito,
Remove ads
Tazama pia
- Carbon cycle
- Rock cycle
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads