Farakano
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Farakano (kutoka kitenzi chenye asili ya Kiarabu; kwa Kiingereza: schism, kutoka neno la Kigiriki σχίσμα, skhisma) ni tendo la kuachana kati ya watu wasioelewana tena baada ya kuwa pamoja. Mara nyingi linahusu taasisi kama vile madhehebu ya dini.
Farakano likishatokea, juhudi za kurudisha umoja mara nyingi zinasababisha mafarakano mapya, kama inavyoonyesha historia ya ekumeni [1].
Ukristo unatofautisha pengine farakano na uzushi[2][3], kwa maana huo unamaanisha tofauti katika mafundisho muhimu ya imani, wakati farakano linaweza kufanyika kwa sababu nyingine, bila tofauti za namna hiyo.
Remove ads
Tanbihi
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads