Fonimu

From Wikipedia, the free encyclopedia

Fonimu ni jina linalotumiwa katika elimu ya fonolojia kwa kutaja sauti bainifu za lugha fulani zilizo sehemu ndogo kabisa za maneno na kuunda tofauti za maana kati ya neno moja na jingine.[1]

Katika Kiswahili

Katika lugha ya Kiswahili tunaweza kutofautisha fonimu za aina tatu:

  • Fonimu za irabu ambazo ni a - e - i - o - u
  • Fonimu za nusuirabu ambazo ni w - y
  • Fonimu za konsonanti ambazo zinaonyeshwa kwa herufi za b - ch - d - dh - f - g - gh - h - j- k - kh - l - m - n - ny - ng' - p - r - s - sh - t - th - v - z; baadhi zinaonyeshwa kwa kuunganisha herufi mbili kama vile dh - kh - ng - ng`- th.

Wataalamu wanatofautiana juu ya idadi ya fonimu za Kiswahili kama ni kwa jumla 33 au 37. [2].

Fonimu huweza kubadili maana ya neno katika lugha husika.

  • mf.-[punga], hapa fonimu [p] ikibadilishwa na kuwekwa fonimu nyingine maana ya neno la awali hubadilika.
  • mf.-[tunga] fonimu [t] imebadili maana ya neno la awali punga

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.