Fungunyota

From Wikipedia, the free encyclopedia

Fungunyota
Remove ads

Fungunyota (kwa Kiingereza: star cluster) ni idadi ya nyota zinazokaa karibu katika anga-nje. Zinashikamana kwa nguvu ya uvutano.[1] Fungunyota maarufu linaloonekana kwa macho ni Kilimia.

Thumb
Fungunyota la Kilimia
Thumb
Fungunyota tufe lenye jina la kisayansi Messier2 jinsi linavyoonekana kwa darubini

Kwa kutumia mitambo ya kisasa wataalamu wa astronomia wamekuta mafungunyota maelfu kadhaa lakini nyingi hazionekani kwa macho matupu au yanaonekana kama nyota ya kawaida tu.

Fungunyota ni tofauti na kundinyota. Katika kundinyota watu wanajumuisha nyota zinazoonekana kukaa karibu na kuwa na umbo maalumu wakitazama anga kwa macho, lakini hali halisi nyota hizo hazina uhusiano kati yao wala hazipo pamoja. Nyingine zipo karibu zaidi na Dunia na nyingine zipo mbali mno. Kinyume chake fungunyota ni kundi la nyota zilizopo karibu hali halisi.

Kwa jumla kuna aina mbili za fungunyota:

  • fungunyota la kawaida ambako kwa kawaida idadi ya nyota haizidi mamia kadhaa. Kilimia ni fungunyota la aina hii lakini ni kati ya nyota sita hadi tisa tu zinazoonekana kwa macho matupu kutegemeana na hali ya anga.
  • fungunyota tufe lina idadi ya nyota maelfu hadi milioni zinazokaa karibu kama tufe kubwa. Chache zao zinaonekana kama nyota kwa macho lakini nyingi zimeonekana tu tangu kupatikana kwa mitambo ya utazamaji ya kisasa.
Remove ads

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads