Mango

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mango (wakati mwingine pia: yabisi[1]) ni moja kati ya hali maada. Maana yake ni imara, tofauti na kiowevu (majimaji) au gesi (kama hewa).

Katika hali mango atomu zinakaa mahali pamoja katika gimba, hazichezi wala kusogea ndani yake. Kila atomu ina mahali pake. Gimba mango lina umbo, mjao na uzani maalumu. Umbo mango lina urefu, upana na kimo chake, tofauti na kiowevu kinachobadilika umbo kufuatana na chombo chake au gesi isiyo na umbo wala mjao maalumu.

Kama mango inabadilika kuwa kiowevu tunasema inayeyuka. Kama inabadilika kuwa gesi au mvuke moja kwa moja tunaliita badiliko hili mvukemango.

Maana ya asili ya "mango" ni jiwe gumu jeusi lililotumika kutwanga kumetesha au kukatua kitu. [2]

Atomi katika hali maada mbalimbali

Tazama pia

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.