Mango
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mango (wakati mwingine pia: yabisi[1]) ni moja kati ya hali maada. Maana yake ni imara, tofauti na kiowevu (majimaji) au gesi (kama hewa).
Katika hali mango atomu zinakaa mahali pamoja katika gimba, hazichezi wala kusogea ndani yake. Kila atomu ina mahali pake. Gimba mango lina umbo, mjao na uzani maalumu. Umbo mango lina urefu, upana na kimo chake, tofauti na kiowevu kinachobadilika umbo kufuatana na chombo chake au gesi isiyo na umbo wala mjao maalumu.
Kama mango inabadilika kuwa kiowevu tunasema inayeyuka. Kama inabadilika kuwa gesi au mvuke moja kwa moja tunaliita badiliko hili mvukemango.
Maana ya asili ya "mango" ni jiwe gumu jeusi lililotumika kutwanga kumetesha au kukatua kitu. [2]
Atomi katika hali maada mbalimbali
- Atomu au molekuli katika hali mango
- Atomu au molekuli katika hali kiowevu
- Atomu au molekuli katika hali ya gesi
Tazama pia
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.