Great Dividing Range

From Wikipedia, the free encyclopedia

Great Dividing Range

Great Dividing Range (kwa maana Mgawanyiko Mkubwa) au Nyanda za Juu za Mashariki, ndiyo safu ya milima kubwa zaidi kwenye bara la Australia [1]. Inaenea kwa kilomita 3,500 sambamba na pwani ya mashariki la Australia, kuanzia Queensland ikipita Victoria hadi magharibi mwa Victoria. Upana wa masafa unatofautiana kutoka karibu km 160 hadi zaidi ya km 300.

Thumb
Milima ya Dividing Range.
Thumb
Ramani ya Australia; rangi njano inaonyesha Great Dividing Range.

Eneo lote si safu moja ya milima tu; kuna safu mbalimbali, milima, nyanda za juu na mitelemko. Kwenye sehemu kadhaa nchi ni karibu tambarare bila miinuko mikubwa, pengine kuna milima mikali inayofikia kimo cha mita 1,600.

Kilele cha juu ni Mlima Kosciuszko wenye mita 2,228 uliopo kwenye milima ya Snowy ("milima ya theluji").

Safu za Great Dividing Range zimepata jina kwa sababu zilikuwa kizuizi cha mawasiliano kati ya mashariki ya Australia ambako idadi kubwa ya wananachi wote inapatikana, na sehemu nyingine za bara.

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.