Hemed Suleiman

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Hemed Suleiman (maarufu kama Hemed Phd) ni msanii wa muziki wa bongofleva na muigizaji wa filamu za bongo maarufu kama Bongo Muvi.

Historia

Hemed Suleiman amezaliwa mwaka 1986 na kakulia jijini Dar es Salaam, alisoma Shule ya Msingi Oyesterbay na baadaye akahamia Shule ya Msingi Bunge kabla ya kujiunga na shule ya Sekondari Annuur Islamic baada ya kumaliza elimu ya kidato cha nne akajiunga na shule ya Eckeneford na baadae akahamia Coastal kwa ajili ya kumaliza kidato cha sita.[1]

Mafanikio

Baada ya kumaliza elimu ya kidato cha sita kipindi anasubiria matokeo akaamua kushiriki shindano la kusaka vipaji vya kuimba la Tusker Project Fame huko nchini Kenya. Shindano hilo lilimfungulia njia ya umaarufu Hemed kiasi kwamba akasahau masomo na kuacha kwenda chuo kikuu. Alishiriki shindano hilo na kushika nafasi ya kwanza.[1]Baada ya kupata umaarufu aliamua kuingia kwenye sanaa ya uigizaji ambako aliamini kwamba angepata umaarufu zaidi. Aliigiza filamu nyingi zilizovuma kipindi hiko na kumpa umaarufu zaidi. Akaigiza filamu nyingi akishirikiana na Jackline Wolper, Yusuf Mlela Jacob Steven au JB na mara kadhaa akaigiza na marehemu mzee Majuto. Kwa ushirikiano mkubwa wakafanikiwa kutengeneza filamu zilizoitambulisha vyema Tansinia ya filamu miongoni mwa wadau wa sanaa hiyo.

Hemed licha ya kuonyesha kipaji chake kwenye uigizaji pia akaamua kuingia kwenye muziki na kuanza kuimba nyimbo za bongofleva. Huku nako akajitahidi kwa kiasi kikubwa kuonyesha uwezo wake na waziwazi akalidhihirisha hilo kwa kutoa nyimbo kali kama vile ‘ Ninachotaka’, imebaki stori, Carolina, Rest of my life. Nyimbo zote hizi zilifanya vyema kwenye soko la muziki ndani na mipaka ya nchi.

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads