Mfalme Hezekia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mfalme Hezekia (kwa Kiebrania: יְחִזְקִיָּ֫הוּ, H̱izkiyyahu, H̱izkiyya, Yeẖizkiyyahu, Ḥizqiyyā́hû, Ḥizqiyyā, Yəḥizqiyyā́hû, Hizqiyyahu ben Ahaz; kwa Kigiriki: Ἐζεκίας, Ezekias) alitawala ufalme wa Yuda kati ya miaka 729 KK na 716 KK pamoja na baba yake mfalme Ahazi, halafu peke yake hadi mwaka 697 KK, tena pamoja na mwanae Manase hadi kifo chake mwaka 687 KK.

Ni mmojawapo kati ya wafalme wachache wanaosifiwa na Biblia kuwa alifanana na mfalme Daudi, babu yake, kwa kuwa alijitahidi kufanya urekebisho wa kidini ili raia zake wamuabudu YHWH tu.
Habari zake zinapatikana hasa katika Kitabu cha Pili cha Wafalme 18-20, Isaya 36-39 na Kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati 29-32, mbali ya kitabu cha Methali 25:1.
Pia anatajwa katika vitabu vya manabii Yeremia, Amosi na Hosea.
Hatimaye anatajwa na Injili ya Mathayo kati ya mababu wa Yesu Kristo.
Anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 28 Agosti.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads