Hoteli

From Wikipedia, the free encyclopedia

Hoteli
Remove ads

Hoteli (kutoka neno la Kiingereza hotel linalotokana na lile la Kifaransa hôtel ambalo, sawa na neno "hospitali", lina asili katika Kilatini hospes, yaani mgeni) ni jengo kubwa lenye vyumba vingi, ambapo watu wanaweza kulala wakati hawapo nyumbani.

Thumb
Hoteli mojawapo.
Thumb
Hoteli ya Llao Llao huko Bariloche (Argentina).

Wenye sehemu hizo wanakodisha chumba kwa siku yoyote. Wanatoa vyumba vya kulala, na kwa kawaida hata chakula, hatimaye kwa ajili ya huduma hizo hutaka pesa, ambazo kiasi chake hutegemea ubora wa jengo.

Pia kuna hoteli ambapo mikutano hufanyika.

Remove ads

Aina za hoteli

Aina za hoteli hulinganishwa na wingi wa vyumba na eneo ambalo hoteli hupatikana.

  • Resort hotel ni aina ya hoteli ambazo hupatikana karibu na mito, maziwa, milima, pembezoni mwa bahari au katika kisiwa, [1]
  • Inn hotel ni aina ya hoteli ambazo mara nyingi hutoa huduma za malazi na kifunguakinywa. [2]
  • Airport hotel ni aina ya hoteli ambazo hupatikana karibu kabisa na viwanja vya ndege na mara nyingi hutoa huduma zake kwa wasafiri wa ndege. [3]
  • Motel hotel ni aina ya hoteli ambazo hupatikana karibu na barabara kubwa na huwa na vyumba vichache kutoa huduma sana kwa madereva wa magari ya watalii. [4]
Remove ads

Aina za vyumba vya hoteli

Aina za vyumba hutazamwa kulingana na aina au idadi ya vitanda vilivyomo ndani yake.

  • Single room ni aina ya chumba maalumu kwa ajili ya kulala mtu mmoja tu[5]
  • Double room ni aina ya chumba maalumu kwa ajili ya watu wawili na huwa na kitanda kimoja kikubwa.
  • Twin bed ni aina ya chumba chenye vitanda viwili vilivyo karibu, wakati mwingine anaweza kulala mtu mmoja katika aina hii.
  • Suite room ni aina ya chumba kikubwa kilicho na sehemu ya kulala pamoja na sebule.
Remove ads

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads