Kanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli (pia Imani ya Nikea) ni fomula rasmi ambayo ilipitishwa na Mtaguso wa kwanza wa Nisea (325)[1] ikakamilishwa na Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli (381) ili kubainisha imani sahihi ya Kanisa Katoliki dhidi ya uzushi, hasa wa Ario na wafuasi wake.


Katima mazingira hayo, lengo kuu lilikuwa kwanza kumkiri Yesu kama Mungu kweli sawa na Baba, halafu kwamba Roho Mtakatifu anastahili kuabudiwa pamoja na Baba na Mwana (Utatu Mtakatifu).
Hadi leo hiyo kanuni ya imani inatumika sana katika madhehebu mengi ya Ukristo, hata kama sehemu ya liturujia.[2][3][4][5][6][7][8][9]
Remove ads
Tafsiri ya Kiswahili
Remove ads
Tofauti kati ya toleo la Nisea na lile la Konstantinopoli
Tunaweza kulinganisha matoleo hayo mawili ya Kigiriki[12] kama ifuatavyo:
Remove ads
Suala la Filioque
Mwishoni mwa karne ya 6, baadhi ya makanisa ya Kilatini yaliongeza neno Filioque (na (kwa) Mwana) yakifundisha kwamba Roho Mtakatifu anatoka kwa Mungu Baba na pia kwa Mungu Mwana. Badiliko hilo lilipingwa na Makanisa ya Kiorthodoksi kama upotoshaji wa imani juu ya mahusiano kati ya nafsi tatu za Mungu [13][14]
Idara husika ya Kanisa Katoliki huko Vatikano iliweka wazi mwaka 1995 kwamba, kama maneno ya Kigiriki καὶ τοῦ Υἱοῦ ("na kwa Mwana") yangeongezwa kwa ἐκπορεύομαι yangekuwa ya kizushi kweli[15][16][17] lakini neno Filioque si la kizushi likiongezwa kwa neno la Kilatini procedit kwa kuwa hilo si sawa na ἐκπόρευμαι[18][19]
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads