Kanuni ya Imani
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kanuni ya imani, au Ungamo la imani, au Tamko la imani, au Nasadiki (Ukristo) au Shahada (Uislamu) ni fomula iliyopangwa kwa muhtasari ili wafuasi wa dini fulani wakiri kwamba wanaamini mafundisho ya dini hiyo.

Katika Uyahudi
Inajadiliwa kama dini ya Uyahudi ina kanuni ya imani. Baadhi wanasema ipo, nayo ni Shema Yisrael (Kumb 6:4), inayoanza hivi: "Sikiliza, ee Israeli: Bwana Mungu wetu, Bwana ni mmoja."
Katika Ukristo
Katika Ukristo ni maarufu hasa Kanuni ya Imani ya Nisea Konstantinopoli, iliyotungwa mwaka 325 katika Mtaguso wa kwanza wa Nisea na kukamilishwa mwaka 381 katika Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli. Ndiyo ya kwanza katika ya Mitaguso ya kiekumene. Msingi wa fomula hiyo ni Agano Jipya lilivyoeleweka kwa kawaida na maaskofu wa Kanisa wa karne ya 4, ambayo ni muhimu sana katika ufafanuzi wa imani uliofanywa na mababu wa Kanisa. Karibu madhehebu yote ya Ukristo yanakubali hadi leo kanuni hiyo.[1]
Pamoja nayo inakubalika sana Kanuni ya Imani ya Mitume iliyotokea Roma katika maadhimisho ya liturujia, hasa ubatizo.
Kabla ya hizo kutungwa, katika Barua ya kwanza kwa Wakorintho (15:3-7) Mtume Paulo aliandika aina ya kanuni ya imani ambayo mwenyewe aliikuta alipoongokea Ukristo akaieneza katika uinjilishaji wake.
Remove ads
Katika Uislamu
Waislamu wanatamka maneno ya shahada kama nguzo mojawapo ya dini yao ili kumkiri Mungu pekee (Allah) na mtume Muhammad kama rasuli wake.[2]
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads