Roboti ya viwandani

From Wikipedia, the free encyclopedia

Roboti ya viwandani
Remove ads

Roboti ya viwandani (kwa Kiingereza: industrial robot) ni mfumo wa roboti unaotumika katika uzalishaji wa bidhaa. Roboti za viwandani ni za kiotomatiki, zinaweza kupangwa na zinaweza kusonga kwa ekseli tatu au zaidi.

Thumb
Seti ya roboti za ekseli sita zinazotumika kuchomelea.

Roboti za viwandani hutumiwa kwa shughuli kama kuchomelea vyuma, kupaka rangi, kuunganisha na kutenganisha, [1] kuchukua na kuweka vipuli kwa bodi za saketi zilizochapishwa, kuweka lebo, ukaguzi wa bidhaa na majaribio; yote yametimizwa kwa kasi, na usahihi. Zinaweza kusaidia katika utunzaji wa nyenzo.

Katika mwaka wa 2020, roboti za viwandani milioni 1.64 zilikuwa zikifanya kazi kote ulimwenguni kulingana na Shirikisho la Kimataifa la Roboti (IFR). [2]

Remove ads

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads