Milioni

From Wikipedia, the free encyclopedia

Milioni
Remove ads

Milioni (1,000,000) au elfu elfu, ni namba ambayo inafuata 999,999 na kutangulia 1,000,001. Inaandikwa pia 106.

Thumb
Kutoka 1 hadi milioni 1 kwa kuzidisha mara kumikumi.

Jina linatokana na lugha ya Kiitalia asili ambapo millione (milione katika Kiitalia cha kisasa) lina mzizi katika neno mille, "1000", likiongezea mnyambuliko -one unaodokeza ukubwa.[1]

Kwa wingi wa milioni kuna kawaida tofauti ya kuzitaja baada ya milioni 999 yaani kuanzia milioni elfu moja au 109. Katika Afrika ya Mashariki wengi hufuata "skeli fupi" inayoita namba hii bilioni moja. Lakini katika vitabu vingi vya Kiingereza vya miaka iliyopita, pamoja na lugha nyingi za Ulaya ,namba hii huitwa "miliardi" na bilioni ni 1012.

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads