Issa Michuzi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Muhidin Issa Michuzi ni mwandishi wa habari wa Tanzania anayejulikana kupitia blogu yake iitwayo Michuzi blog. [1]
Maisha yake na kazi
Michuzi tangu zamani alikuwa akipendelea kazi ya upigaji picha. Mnamo mwaka 1980 alijiunga na vipindi vya jioni katika taasisi iitwayo Dar es Salaam. Moja kati ya picha alizowahi kupiga ilichaguliwa kwa ajili ya kurasa ya mwanzo wa gazeti la Daily News linalomilikiwa na serikali ya Tanzania.
Baada ya hapo aliajiriwa kwa mkataba wa muda mfupi kama ripota kwa muda wa miaka mitatu kabla ya kuajiriwa kwa mkataba wa muda mrefu Januari mwaka 1990.[2]
Mwaka 1992 alijiunga na Chuo cha Uandishi wa Habari cha Ujerumani mjini Berlin Kwa masomo ya juu ya uandishi wa habari.Baadae alijiunga na chuo cha uandishi wa habari (present-day School of Journalism and Mass Communication) kilichopo University of Dar es Salaam na kumalza mwaka 1996.
Remove ads
Kazi yake ya uandishi
Mnamo Septemba 2005, Michuzi aliungana na Jakaya Kikwete ambaye kwa wakati huo alikuwa Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania aliyekuwa akihudhuria Mkutano wa Mchakato katika Utandawazi na Demokrasia mjini Helsinki nchini Finland. Huko likutana na Ndesanjo macha aliemsaidia kuandaa blogi yake.Blogi yake ya kwanza ailitengenezwa tarehe 8 seotemba mwaka 2005. [3] .Madhumuni yake yalikua kuwataarifu Watanzania kuhusu habari zinazohusu nchi yao kwa kupitia blogu za picha.
Remove ads
Maisha binafsi
Michuzi ana kaka wawili, Ahmaad na Othman amabo pia wanashughulika na kazi zao na uandishi Tanzania.Kwa pamoja wametengeneza blogi iitwayo michuzi media Group (MMG).
Ni mpenzi wa muziki wa Tanzania bongo flava ni shabiki wa timu ya Liverpool F.C..
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads