Jack the Ripper

From Wikipedia, the free encyclopedia

Jack the Ripper
Remove ads

Jack the Ripper ni jina la kumtaja muuaji asiyejulikana kwa jina halisi ambaye aliua kinyama malaya angalau watano mjini London wakati wa mwaka 1888. Mauaji yote yalitokea katika mtaa wa Whitechapel kuanzia 31 Agosti hadi 9 Novemba 1888. Wakati ule barua zilifika magazetini na katika ofisi za polisi ambako waandishi walijivuna kuwa mtendaji wa mauaji haya na mwandishi mmoja alitia sahihi "Jack the Ripper". Magazeti yaliandika mengi juu ya mauaji ya mfululizo yaliyofanana na hivyo jina la "Jack the Ripper" lilikuwa maarufu sana. Majina mengine yaliyotumiwa wakati ule ni "Whitechapel Murderer" na "Leather Apron" (yaani "aproni ya ngozi") lakini umaarufu wa "Jack the Ripper" umebaki hadi leo.

Thumb
Mchoro katika gazeti la "The Illustrated London News", 13 Oktoba 1888, inayojaribu kuonyesha picha ya muuaji
Remove ads

Mazingira ya mauaji.

Wakati ule London ilikuwa mji uliokua haraka sana. Sehemu ya Whitechapel ilikuwa n]]a wahamiaji wengi kutoka Ulaya bara hasa Ulaya ya Mashariki na kati yao Wayahudi wengi waliokimbia mashambulio ya pogromu dhidi ya Wayahudi katika Urusi[1]. Wengi walikuwa maskini waliokosa makaazi na kulala katika mabweni ya kukodi. Uhalifu na wizi zilitokea kwa wingi katika mazingira haya[2]. Wanawake wengine kati ya wahamiaji walitafuta riziki kwa njia ya umalaya. Taarifa za mashambulio dhidi ya wanawake zilizidi. Wakati wa Oktoba 188 polisi ilikadiria kuwepo kwa nyumba 62 za danguro na takriban wanawake 1,200 waliofanya kazi ya umalaya katika mtaa wa Whitechapel[3].


Thumb
Ramani ya London ya miaka ya 1880 na alama zinaonyesha mahali pa mauaji 7 yaliyotokea katika mazingira ya mitaa michache (kesi 5 za uhakika na 2 zenye shaka kama zilikuwa kazi ya Jack the Ripper).
Remove ads

Mauaji ya 1888 katika Whitechapel

Wanawake watano wanaodhaniwa kuwa wahanga wa "Jack the Ripper" walikuwa wafuatao

  • Mary Ann Nichols mwenye umri wa miaka 47, tarehe 31 Agosti
  • Annie Chapman mwenye umri wa miaka 42, tarehe 8 Septemba
  • Elizabeth Stride mwenye umri wa miaka 44, tarehe 30 Septemba
  • Catharine Eddowes mwenye umri wa miaka 46, tarehe 30 Septemba
  • Mary Jane Kelly mwenye umri wa miaka 25, tarehe 9 Novemba

Kulikuwa na maujai zaidi na polisi ilichungulia jumla ya kesi 11 zilizotokea Whitechapel kati ya Aprili 1888 na Februari 1891. Mawazo yalitofautiana kama zote zilitekelezwa na muuaji yeye yule. Lakini kesi tano zinazotajwa hapo juu zinaonyesha dalili za kusababishwa na mtu mmoja. Kati ya dalili hizi ni kukatwa kwa shingo, kufunguliwa kwa tumbo na kukatakata sehemu za uke na uso, pamoja na kutoa ogani za utumbo. [4]

Kwa jumla muuaji katika kesi hizi alipendelea kuua wahanga wakati wa usiku baina ya saa sita na saa kumi na mbili kwenye siku za wikendi. Mauaji haya yalitokea katika eneo la maili moja ya mraba. Maiti zilipatikana mahali walipouawa, hawakupelekwa mahali pengine[5]. Silaha ya mauaji ilikuwa kisu kikali. Wahanga waliuawa kwa njia ya kunyonga kabla ya kukatwa shingo.

Idadi kamili ya mauaji ya "Jack the Ripper" haijulikani. Maana wakati ule kulikuwa pia na mauaji mengine yasiyofanana kabisa na mtindo ulioonekana katika kesi 5 za uhakika zaidi. Kesi chache zilifanana kiasi au kidogo tu na hapo watafiti walijiuliza kama labda muuaji alikosa muda wa kumaliza alichotaka kutekeleza au kama mifano hii ilikuwa matendo ya watu wengine.[6]

Polisi ilifanya utafiti kesi tofauti 11 za mauaji ya wanawake katika Whitechapel kuanzia 3 Aprili 1888 hadi 13 Februari 1891 kwa jina la "mauaji ya Whitechapel".[7][8]


Remove ads

Barua

Wakati habari za mauaji haya yalisambazwa magazetini kulikuwa na barua nyingi zilizofika kwa polisi au magazeti. [9] Barua hizi zilileta maoni namna ya kumshika muuaji, au maoni mbalimbali juu ya jinai hizi. [10]

Barua nyingi zilitungwa kwa kudai kuwa muuaji mwenyewe aliziandika.[11] na tatu kati ya hizi nyingi zimepata umaarufu: barua iliyoandikwa kwa "Dear Boss", kadi ya "Saucy Jacky" na barua "kutoka jahanam (From Hell letter).[12]

Barua inayoanza kwa maneno "Dear Boss" ya tarehe 25 Septemba yenye mhuri wa posta ya 27 Septemba 1888 ilipokelewa na shirika la habari la Central News Agency (London) na kupelekwa polisi ya Scotland Yard.[13] Mwanzoni ilitazamiwa kuwa mzaha mbaya lakini siku tatu baada ya tarehe ya mhuri wa barua maiti ya Eddowes ilipatikana na sehemu ya sikio ilikatwa. Hapa polisi iliangalia barua upya kwa sababu ilikuwa na maneno "masikio ya wakinamama yataktwa". [14] Barua hii ilitumia mara ya kwanza sahihi "Jack the Riper" na jina hili lilikuwa maaraufu baada ya kuchapishwa kwa barua magazetini.[15] Haikueleweka kama iliandikwa kweli na muuaji kwa sababu sikio halikutumwa kwa polisi jinsi barua iliwahi kutangaza.

Barua nyingi zilizofuata zilijaribu kuiga mfano huu hata kama ilikuwa wazi ziliandikwa na watu tofauti kutokana na maandishi [16]

Thumb
Barua ya "Kutoka Jehanamu" (From Hell).

Postikadi ya "Saucy Jacky" iligongwa mhuri tarehe 1 Oktoba 1888 na kupokelewa siku ileile katika Central News Agency. Maandishi yalifanana na yale ya barua ya "Dear Boss" letter.[17] Ilirejea ya kwamba wahanga wawili waliuawa kwenye siku za karibu ("double event this time") na hii ilichukuliwa kama kurejea mauaji ya Stride and Eddowes.[18] Postikadi hii ilipelekwa posta kabla ya kutangazwa kwa mauaji aya mawili kwa hiyo mjanja aliyetaka kufanya mzaha asingekuwa na habari. [19].

Barua "From Hell" ilipokelewa na George Lusk kiongozi wa kamati ya ulinzi ya Whitechapel tarehe 16 Oktoba 1888. Maandishi hayakufanana na yale ya barua ya "Dear Boss" na postikadi ya "Saucy Jacky".[20] Ilifika pamoja na kisanduku chenye nusu ya figo iliyotunzwa katika alkoholi ethili.[20] Maiti ya Catharine Eddowes ilikutwa tarehe 30 Septemba ilhali figo moja ilikosekana. Mwandishi wa barua aliandika ya kwamba aliwahi kula nusu nyingine ya figo. Ndani ya polisi mawazo yalitofautiana kuhusu kipande cha figo. Wengine waliona ni ya Eddowes, wengine walidhani hii ni mzaha mbaya.[21][22] Utafiti wa figo ulionyesha kuwa ilikuwa figo la kibinadamu la upande wa kushoto.[23]

Polisi ya Scotland Yard ilitangaza kopi za barua ya "Dear Boss" na postikadi kwa tumaini ya kwamba msomaji angetambua maandishi ya mkono lakini bila mafanikio. Afisa mkuu wa polisi ya London Charles Warren aliamini ya kwamba barua zote zilikuwa mzaha [24]. Wengine waliona ya kwamba barua ziliandikwa na waandishi wa magazeti kwa shabaha ya kuuza nakala nyingi. [25] [26] Mwaka 1931 mwandishi wa gazeti Fred Best alisemekana ya kwamba aliwahi kutunga barua na kutia sahihi "Jack the Ripper" kwa shabaha ya kuboresha biashara ya gazeti lake. [27]

Remove ads

Marejeo

Kujisomea

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads