John Wayne
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Marion Mitchell Morrison (26 Mei 1907 – 11 Juni 1979) amezaliwa na jina la Marion Robert Morrison, lakini anajulikana sana kwa jina la kisanii kama John Wayne, alikuwa mwigizaji wa filamu, mwongozaji, na mtayarishaji kutoka nchini Marekani. Anafahamika sana kwa sauti yake chini-chini, utembeaji na urefu. Pia alifahamika kwa michango yake ya kimawazo juu ya siasa na kuunga mkono kwake sera za kupinga-ukomunisti.
Toleo la Harris Poll la mwezi wa Januari 2009 limemweka Wayne sehemu ya tatu akiwa kama moja kati ya manyota wa filamu wenye wapenzi huko nchini Marekani,[1] nyota pekee aliyekufa na kuonekana kwenye orodha yao kila mwaka tangu kuanza kutolewa kwake mnamo mwaka wa 1994.
Mnamo mwaka wa 1999,Taasisi ya Filamu ya Marekani imempa Wayne nafasi ya 13 kwenye orodha yao ya Waigizaji Wakali wa Kiume wa Muda Wote.
Remove ads
Maisha ya awali
Wayne alizaliwa na jina la Marion Robert Morrison mjini Winterset, Iowa.[2] Jina lake la kati lilibadilishwa mapema kutoka Robert na kuwa Mitchell pale wazazi wake walipoamua kumwita mtoto wao aliyefuatia jina la Robert. Familia yake walikuwa Wapresbyteri. Baba yake, Clyde Leonard Morrison, (1884–1937), alikuwa na asili ya Kiere, Mskoti-Mweire na Mwingereza, na ni mtoto wa mkongwe aliyepigana Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Marekani Bw. Marion Mitchell Morrison (1845–1915). Mama yake, zamani Mary Alberta Brown (1885–1970), alikuwa anatokea Lancaster County, Nebraska.
Familia ya Wayne ilihamia mjini Palmdale, California, na mnamo 1911 wakaelekea zao mjini Glendale, California, ambapo baba yake alifanya kazi kama mfamasia. Mzima moto mmoja kwenye kituo hicho wakati John yuko katika safari zake za kila siku za kuelekea shule huko Glendale akaanza kumwita "Little Duke", kwa sababu alikuwa haendi popote bila ya jibwa lake kubwa la Airedale Terrier, Duke.[3][4] Yeye akapendekeza "Duke" kuwa badala ya "Marion," na jina hilo likamkaa kwa maisha yake yote.
Remove ads
Marejeo
Soma zaidi
Viungo vy Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads