Jux

Mwanamuziki wa kitanzania From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Juma Mussa (anajulikana kwa jina la kisanii Jux; amezaliwa 1 Septemba, 1989) ni mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania. Ana asili mchanganyiko kutoka Lindi na Morogoro.

Jux alianza kuvuma kwa nyimbo zake za Nimedata, Mwambie, Uzuri Wako, Nitasubiri, Sisikii, Juu na Utaniua.

Jux ni msanii wa R&B aliyefanya video zake nyingi nchi za nje kushinda wasanii wengi wa R&B nchini Tanzania.

Aliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Vanessa Mdee uliodumu kwa miaka takribani 7. Kwa sasa mwanamuziki Jux ana mahusinano na Priscilla Ojo ambaye ni mwanamitindo, mwigizaji na msawishi maarufu kutoka Nigeria.

Remove ads

Mafanikio

Tuzo ya Best collaboration Of The Year Akiwa Amshirikisha Msanii Diamond Platnumz kupitia nyimbo ya Enjoy.

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads