Mkoa wa Morogoro

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mkoa wa Morogoro
Remove ads

Mkoa wa Morogoro ni mmojawapo ya mikoa ya Tanzania uliopo katikati ya mashariki mwa Tanzania, ukiwa na makao makuu mjini Morogoro. Unapakana na Mkoa wa Tanga upande wa kaskazini-mashariki, Mkoa wa Manyara kaskazini, Mkoa wa Dodoma kaskazini-magharibi, Mkoa wa Iringa upande wa kusini-magharibi, Mkoa wa Njombe, mkoa wa Ruvuma na mkoa wa Lindi kusini, na Mkoa wa Pwani upande wa mashariki. Eneo lake ni km² 72 939, ambapo kuna wakazi 3,197,104 kadiri ya sensa ya mwaka 2022 [1] na kuwa kati ya mikoa mikubwa na yenye wakazi wengi zaidi ya Tanzania. Una Hifadhi ya Taifa ya Mikumi na Milima ya Uluguru, na ni lango la kuelekea Milima ya Udzungwa na Hifadhi ya Taifa ya Nyerere. Mkoa huo ni maarufu kwa shughuli za kilimo, hasa cha miwa, mahindi, mpunga, na mazao ya matunda, pamoja na viwanda vya kusindika mazao hayo. Pia una nafasi muhimu katika elimu na mafunzo kupitia taasisi mbalimbali kama Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).

Ukweli wa haraka Nchi, Wilaya ...
Thumb
Mnara wa saa, Morogoro
Remove ads

Jiografia

Eneo la Mkoa wa Morogoro liko katikati ya mikoa ya pwani ya Bahari Hindi na Nyanda za Juu za Kusini Tanzania.

Kuna tambarare za chini kama vile Ifakara / Kilombero, pia milima ya juu kama Uluguru yenye mlima wa Kimhandu wenye kimo cha mita 2,646 juu ya UB.

Mito mikubwa ni Wami na Ruvu inayoanza kwenye milima ya Uluguru. Ruvu ndio mto wa kutoa maji kwa wakazi wa Dar es Salaam.

Karibu nusu ya eneo la Mkoa wa Morogoro ni hifadhi za taifa za Mikumi na sehemu ya eneo la Hifadhi ya Taifa ya Nyerere na la ile ya Udzungwa.

Remove ads

Utawala

Mkoa una wilaya tisa ambazo ndizo (katika mabano idadi ya wakazi mwaka 2022): Gairo (268,205), Kilosa (617,032), Malinyi (225,126), Mlimba (292,536), Morogoro Vijijini (387,736), Morogoro Mjini (471,409), Mvomero (421,741), Ulanga (232,895).

Wakazi walio wengi hukalia wilaya za kaskazini. Zaidi ya robo huishi katika miji ya mkoa.

Maelezo zaidi Ramani, Wilaya au manisipaa ...
Remove ads

Wakazi

Kabila kubwa ni la Waluguru waliotoa jina kwa mji wa Morogoro pamoja na milima ya Uluguru.

Makabila mengine makubwa zaidi ni Wangulu, Wakagulu, Wasagala, Wapogolo, Wandamba, Wabena, Wambungu, Wakutu na Wavidunda.

Upande wa dini, karibu nusu ni Waislamu na nusu ni Wakristo.

Mawasiliano

Barabara Kuu za lami za Dar es Salaam - Morogoro - Mbeya - Zambia/Malawi na Dar es Salaam - Morogoro - Dodoma hupita makao makuu ya mkoa pamoja na reli ya kati Dar es Salaam - Morogoro - Dodoma - Kigoma / Mwanza na reli ya SGR Tanzania Dar es Salaam - Morogoro - Dodoma. Reli ya TAZARA hupita wilaya ya Mlimba.

Uchumi

Thumb
Matunda aina ya maembe yakiwa mtini huko Morogoro

Ardhi ya Morogoro ina rutuba ya kufaa kwa mazao mengi. Lakini kilimo kinategemea hali ya mvua.

Karibu nusu ya eneo la mashamba yote hulimwa mahindi.

Mazao ya sokoni hulimwa milimani.

Mkoa wa Morogoro ni eneo lililojaliwa na Mungu kwa uzalishaji wa sukari kwa wingi. Hasa Wilaya ya Mlimba ina mashamba makubwa ya miwa.

Majimbo ya bunge

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

  • Gairo : mbunge ni Ahmed Shabiby (CCM)
  • Kilombero : mbunge ni Peter Lijualikali (Chadema)
  • Kilosa : mbunge ni Baraka Bawazir (CCM)
  • Mikumi : mbunge ni Joseph Haule (Chadema)
  • Mlimba : mbunge ni Suzan Kiwanga (Chadema)
  • Morogoro Kusini : mbunge ni Prosper Joseph Mbena (CCM)
  • Morogoro Kusini Mashariki : mbunge ni Omar Tibweta Mgumba (CCM)
  • Morogoro Mjini : mbunge ni Abood Mohamed Abdul Aziz (CCM)
  • Mvomero : mbunge ni Ahmed Sadiq Murad (CCM)
  • Ulanga Magharibi/ Malinyi : mbunge ni Dk. Hadji Mponda (CCM)
  • Ulanga Mashariki : mbunge ni Goodluck Mlinga (CCM)
Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads