K-Ci

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

K-Ci (alizaliwa na jina la: Cedric Renard Hailey; alizaliwa 2 Septemba, 1969) ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka nchini Marekani. Anajulikana zaidi kama mwimbaji mkuu wa kundi la Jodeci na mwimbaji wa pili katika duo la kindugu la K-Ci & JoJo. Kabla ya umaarufu wake katika muziki wa R&B, alianza kama mwimbaji wa injili akiwa na kaka yake JoJo katika kundi la Little Cedric and the Hailey Singers.

Ukweli wa haraka Jina la kuzaliwa, Pia anajulikana kama ...
Remove ads

Maisha ya awali

K-Ci alizaliwa mjini Charlotte, North Carolina, kwa wazazi Anita na Cliff Hailey, wote wakiwa waimbaji wa injili. Familia yao iliishi kwa muda Baltimore kabla ya kurejea Charlotte alipokuwa kijana. Alisoma katika shule ya sekondari ya Garinger.

Kazi ya muziki

K-Ci alianza kurekodi muziki wa injili na kaka yake Joel (JoJo) na baba yao, wakitoa albamu tatu kati ya 1983 na 1985. Baadaye walikutana na ndugu wengine wawili akina DeGrate (DeVante Swing na Dalvin), na kuunda kundi la R&B la Jodeci. K-Ci alikuwa mwimbaji mkuu wa kundi hilo, ambalo lilitoa albamu tatu zilizopata mafanikio makubwa kati ya 1991 na 1995. Baada ya Jodeci kuchukua mapumziko mwaka 1996, K-Ci aliendelea kufanya kazi na JoJo kama duo la kindu la K-Ci & JoJo, wakitoa albamu tano kati ya 1997 na 2013.

Kama msanii wa kujitegemea, K-Ci alirekodi wimbo maarufu wa Bobby Womack "If You Think You're Lonely Now" mwaka 1994, ambao ulifika nafasi ya 17 kwenye chati ya Billboard Hot 100. Pia alishirikiana na Mary J. Blige katika wimbo "I Don’t Want to Do Anything" kwenye albamu yake ya kwanza What's the 411? (1992).

Remove ads

Maisha binafsi

K-Ci aliwahi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Mary J. Blige kati ya 1992 na 1997. Ingawa Blige alidai walikuwa wamechumbiana, K-Ci alikanusha kuwa walikuwa na mpango wa kufunga ndoa. Yeye na JoJo ni binamu wa wasanii wengine wa R&B kama Fantasia Barrino, Dave Hollister, Calvin Richardson, na Stephanie Mills.

Albamu akiwa na Jodeci

Maelezo zaidi Mwaka, Jina la Albamu ...

Albamu akiwa na K-Ci & JoJo

Maelezo zaidi Mwaka, Jina la Albamu ...

Albamu za K-Ci kama msanii wa kujitegemea

Maelezo zaidi Mwaka, Jina la Albamu ...

Nyimbo maarufu za solo

  • "If You Think You're Lonely Now" (1994) – kutoka kwenye filamu Jason's Lyric
  • "I Don’t Want to Do Anything" (1992) – aliimba na Mary J. Blige

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads