Kahama (mji)

Mji uliopo nchini Tanzania From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Kahama ni manisipaa[1] iliyo kaskazini magharibi mwa Tanzania na yalipo makao makuu ya wilaya ya Kahama Mjini katika Mkoa wa Shinyanga, wenye halmashauri yake ya pekee hivyo yenye hadhi ya wilaya. Halmashauri ilianzishwa baada ya kugawa Wilaya ya Kahama ya awali.

Ukweli wa haraka Nchi, Mkoa ...
Remove ads

Mahali ilipo

Kahama ipo takriban kilomita 109 (sawa na maili 68) umbali kwa barabara kutokea kusini magharibi mwa Shinyanga ambapo makao makuu ya mkoa yanapatikana.[2] pia ni takriban kilomita 536 sawa na maili 333 umbali kwa barabara kutokea kaskazini magharibi mwa Dodoma ambao ndio mji mkuu wa Tanzania.[3]

Idadi ya watu

Mwaka 2006 ilikadiriwa kuwa na idadi ya watu 36,000.[4]

Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa watu 242,208. [5] na katika ile ya mwaka 2022 walihesabiwa 453,654 [6].

Mji huu ni maarufu kwa uchimbaji wa dhahabu. Pia ni mji wa pili kwa mapato kati ya halmashauri za wilaya, ikitanguliwa na Kinondoni na kufuatiwa na Mufindi.

Tangu 1984 mji umekuwa makao makuu ya dayosisi ya Kahama ya Kanisa Katoliki.

Remove ads

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads