Kaliningrad Oblast

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kaliningrad Oblast
Remove ads

Kaliningrad Oblast (rus. Калининградская область kalinin-grad-skaya oblast) ni jina la kutaja mkoa wa Urusi. Mji mkuu wake ni Kaliningrad (hadi 1945 Königsberg).

Thumb
Sehemu ya mkoa wa Kaliningrad Oblast
Thumb
Mahali pa Kaliningrad Oblast katika Russia
Thumb

Eneo la Kaliningrad Oblast liko nje ya Urusi penyewe kati ya Polandi na Lithuania.

Hadi mwaka 1945 ilikuwa sehemu ya jimbo la Prussia Mashariki katika Ujerumani. Kwenye mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia lilivamiwa na jeshi la Umoja wa Kisovyeti, wakazi Wajerumani walikimbia au walifukuzwa na mwaka 1946 eneo hili liliingizwa katika Jamhuri ya Kisovyieti ya Kirusi. Hata baada ya kuporomoka kwa Umoja wa Kisovyeti mnamo mwaka 1991 eneno lilibaki sehemu ya Urusi.

Kisiasa eneo lina umuhimu mkubwa kutokana na bandari yake ya jeshi la majini wa Urusi na vituo vya roketi za kijeshi.

Kiuchumi wakazi wengi wanaona matatizo hasa kutokana na hali ya Kaliningrad ya kuwa mbali na taifa mama ikiviringishwa pande zote na nchi ambazo ni wanachama wa Umoja wa Ulaya.

Kuna wakazi wapatao 942,000 (2010) na eneo lake ni km² 15,125.

Remove ads

Tazama pia

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu maeneo ya Urusi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kaliningrad Oblast kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads