Mkoa wa Kasai Mashariki
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kasai Mashariki (Kasai-Oriental kwa Kifaransa) ni mmojawapo kati ya mikoa 26 ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Kasai-Oriental ni kati ya maeneo duniani yenye almasi nyingi.
Makao makuu ya mkoa ni Mbuji-Mayi.
Jina la mkoa linatokana na mto Kasai.
Remove ads
Historia
Kasai-Oriental inakaliwa hasa na Waluba. Kabla ya ukoloni sehemu kubwa za mkoa zilkuwa chini ya milki ya Luba.
Wakati wa uhuru wa Kongo wanasiasa wa sehemu hii walijaribu kuanzisha dola la kujitegemea la Kasai kusini lakini jeshi la serikali kuu lilivamia eneo lake. Baada ya vita ya miezi minne iliyokuwa na wahanga kwa maelfu eneo lilirudishwa Kongo na kugawiwa.
Lugha
Kifaransa ni lugha rasmi. Tshiluba ni lugha inayotumiwa na wakazi wengi na ni moja ya lugha za kitaifa za Kongo.
Wilaya
Mkoa umegawanywa katika mi wa Mbuji-Mayi na wilaya 5:
Almasi
Eneo la mji wa Mbuji-Mayi linazalisha asilimia 10 ya almasi zote zinazotolewa duniani. Uchimbaji unasimamiwa na kampuni ya Société Minière de Bakwanga, ingawa wananchi wengine wanajaribu kuchimba almasi kibinafsi. Kwa jumla wakazi wa mkoa hawafaidiki na utajiri huo.
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads