Katekisimu

From Wikipedia, the free encyclopedia

Katekisimu

Katekisimu (pia katekesimo; kwa Kigiriki κατηχισμός, katekismos, kutokana na maneno kata = "chini" + echein = "kusikika" masikioni) ni kitabu chenye muhtasari wa mafundisho ya imani na maadili ya Kikristo. "Katekisimu" ni tahajia ya kawaida kwa Wakatoliki, "katekesimo" ni tahajia upande wa Waprotestanti.

Thumb
Codex Manesse, fol. 292v, "Mwalimu wa Esslingen" (Der Schulmeister von Eßlingen)
Thumb
Kipindi cha katekesi huko India, 1939.

Historia

Vitabu vya namna hiyo vinatumika toka karne za kwanza za Kanisa la Magharibi hasa kwa kuandaa watu kupokea ubatizo na sakramenti nyingine.[1]

Mara nyingi mafundisho hayo yanatolewa kwa namna ya majibizano, yaani maswali yakifuatwa na majibu ambayo yanafaa kukaririwa.

Wakati wa matengenezo ya Kiprotestanti, katekesimo ndogo ya Martin Luther, pamoja na katekesimo kubwa, ilijumlisha mafundisho ya kimsingi kwa wafuasi wake.

Wakati huo hata Wakatoliki walitunga katekisimu mbalimbali; maarufu zaidi ni ile ya Petro Kanisi.

Katekisimu ya Kanisa Katoliki, iliyotolewa na Papa Yohane Paulo II kufuatana na Mtaguso wa pili wa Vatikano, ndiyo katekisimu rasmi ya Kanisa hilo na ndiyo inayotumika zaidi duniani siku hizi.

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.