Keir Starmer
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Sir Keir Rodney Starmer (amezaliwa 2 Septemba 1962) ni mwanasiasa na wakili wa Uingereza ambaye amehudumu kama Waziri Mkuu wa Uingereza tangu 5 Julai 2024, na amekuwa kiongozi wa 19 wa Chama cha Labour tangu mwaka 2020.[1] Pia aliwahi kuwa Kiongozi wa Upinzani kutoka 2020 hadi 2024. Tangu mwaka 2015, amekuwa Mbunge wa Holborn na St Pancras, jimbo la ndani ya London. Starmer amechaguliwa tena kama Mbunge wa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu wa 2017 na wa 2019.

Remove ads
Kiongozi wa Labour
Mnamo Januari 2020, Starmer alitangaza kugombea nafasi ya Kiongozi wa Chama cha Labour katika uchaguzi wa 2020.[2] Mnamo 4 Aprili 2020, Starmer alichaguliwa kuwa kiongozi wa Chama cha Labour, na kwa kuwa Labour ilikuwa na idadi ya pili ya viti katika Bunge la Commons, alifanywa kuwa Kiongozi wa Upinzani.[3] Alishinda uongozi wa Chama cha Labour katika raundi ya kwanza ya upigaji kura kwa kutumia mbinu ya kura inayoweza kuhamishwa. Starmer alipata kura 275,780 (56.2%). Alipata asilimia 53.13% ya kura za wanachama wa vyama washirika, asilimia 56.07% ya kura za wanachama wa Chama cha Labour, na asilimia 78.64% ya kura za wafuasi waliosajiliwa.[4]
Remove ads
Maisha binafsi
Starmer ni haamini uwepo wa Mungu,[5] lakini amesema kuwa anaamini katika imani na nguvu yake ya kuwaleta watu pamoja. Mke wake, Victoria Alexander, ni Myahudi, na watoto wao wawili wanalelewa katika imani hiyo.[6]
Marejeo
Viungo vya Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads