Kidaku

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kidaku
Remove ads

Vidaku ni ndege wadogo wa jenasi Melaenornis katika familia Muscicapidae. Spishi kadhaa ziliainishwa katika jenasi Bradornis na Dioptrornis lakina jenasi hizi zimeunganishwa na Melaenornis sasa. Spishi moja inaitwa chekiro. Ndege hawa wana rangi kijivu na/au nyeusi. Wanatokea misitu na maeneo mengine yenye miti katika Afrika. Hula wadudu. Kwa kawaida vidaku hukaa tawi wakiangalia ujirani. Wakiona mdudu huruka ili kumkamata na kurudi tawi. Hujenga tago lao kwa umbo wa kikombe katika tundu la mti au dhidhi ya shina. Jike huyataga mayai 2-6.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Remove ads

Spishi

Remove ads

Picha

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads