Kikuba

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Kikuba ni pambo la manukato linalotengenezwa kwa kuchanganya maua mbalimbali yakunukia pamoja na majani.

Maua yanayotumika ni kama vile asumini, vilua na mawaridi, majani yanayotumika ni kama vile mkadi na mrehani, kwa ustadi wa hali ya juu, majani na maua hayo huunganishwa pamoja kwa kutumia sindano na uzi.

Kibuba hupachikwa kwenye mto wa kulalia, mabegani, kichwani na hata kifuani na huwa na harufu nzuri sana.

Utengenezaji wa vikuba mbali ya kuwa ni sanaa ya hali juu pia ni chanzo cha ajira kwa wengi mjini Mombasa.

Bei ya kikuba hulingana na ukubwa wake.Kikuba cha bei ya chini kabisa ni huanzia shilingi mia tatu hivi.

Kikuba ni tunu kwa mwanamke wa Pwani na hutumika hususan na wanamke  waliolewa, ili kunogesha penzi kwenye ndoa.

Unaweza kumtunuku kikuba swahiba yako, wifi na mavyaa, wengine hujifurahisha kwa raha zao.

Kikuba sio pambo tu bali ni tunu ya utamaduni na uchumi wa Mombasa.

Mombasa Raha!

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kikuba kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads