Marashi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Marashi
Remove ads

Marashi (kutoka kitenzi chenye asili ya Kiarabu "kurasha"; kwa Kiingereza "perfume") ni mchanganyiko wa mafuta na manukato yanayonukia vizuri ambayo hupulizwa au kupakwa katika mwili, nguo, viatu au hata nyumba. Marashi hufanya kunukia vizuri hata pahala palipokuwa pakinuka vibaya.

Thumb
Uandaaji wa marashi nchini Misri, karne ya 4 KK.

Maandishi ya kale na yaliyovumbuliwa na wasomi wa akiolojia yaonyesha kwamba utumiaji wa marashi umekuwako kwa muda mrefu sana.

Utumiaji wa marashi ya kisasa ulianza katika karne ya 19 baada ya kutengenezwa kwa vitu kama vanilin na coumarin.

Remove ads

Historia ya marashi

Utengenezaji wa marashi ulianzia nchini Mesopotamia na Misri na baadaye kuboreshwa katika nchi za Warumi na Persia.

Mtengenezaji wa kwanza wa marashi yaaminika alikuwa mwanamke aliyebobea katika somo la Kemia. Kwa jina aliitwa Tapputi. Ametajwa katika maandishi ya kale ya Mesopotamia. Alitengeneza marashi kwa kuchanganya maua yaliyopondwapondwa, mafuta, calamus na manukato mengine. Mchanganyiko huo aliuchunga na kuuweka kwa muda.

Utumizi wa marashi leo

Marashi ya leo hutengenezwa kwa kutumia maua, asali, ngozi za miti pamoja na kemikali zilizotengenezwa katika maabara.

Marashi hutumiwa kwa kupuliza miili kuondokana na harufu mbaya, kupuliza viatu shoe deodorizers ili yaache kunuka, pamoja na kupuliza kwa nyumba kama air fresheners.

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads