Kituo cha angani

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kituo cha angani
Remove ads

Kituo cha angani (kwa Kiingereza: Space station) ni satelaiti inayozunguka Dunia kwenye njiamzingo ya kudumu ikibuniwa kubeba wanaanga. Kusudi lake ni kuwezesha wanaanga kukaa kwenye anga-nje kwa kipindi fulani na kuendesha utafiti wa kisayansi wa aina mbalimbali. Kinaweza kutembelewa na vyombo vya angani kama feri ya anga na kwa njia hiyo wanaanga wanaweza kufika au kurudi duniani na kupokea vifaa, fueli na chakula.

Thumb
Kituo cha angani cha MIR, mnamo 1995

Tangu mwaka 2000 kuna Kituo cha Angani cha Kimataifa. Kilitanguliwa na vituo mbalimbali kama vile MIR (Urusi), Skylab (Marekani) na Tiagong (China).

Shabaha ya vituo vya angani ni kuchunguza athira ya hali pasipo mvutano kwa mwili na nafsi ya binadamu na kutumia maabara zake kwa majaribio ya kisayansi[1]. Wanaanga hukaa kwa wiki au miezi kadhaa. Mwanaanga aliyekaa kwenye kituo cha angani kwa muda mrefu zaidi alikuwa Valeriy Polyakov (siku 437 kwenye MIR)[2]. [3].

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads