Kivinjari cha simu

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kivinjari cha simu
Remove ads

Kivinjari cha simu (pia: kidurusu cha simu) ni programu inayoruhusu mtu kuvinjari tovuti kwenye simujanja, PDA, au kishikwambi (tablet). Kivinjari hiki kimebuniwa kwa namna inayowezesha kurasa za mtandao kuonekana vizuri kwenye skrini ndogo za vifaa vya mkononi.

Thumb
Ukurasa wa Wikipedia kwenye iPhone 2G kupitia kivinjari cha Safari

Baadhi ya vivinjari vya simu, hasa vile vya zamani, viliundwa kuwa vyepesi na vyenye matumizi madogo ya kumbukumbu na data ili kuweza kufanya kazi kwenye simu zenye uwezo mdogo wa kuhifadhi data na kasi ya mtandao isiyo kubwa. Simu ndogo za zamani zilikuwa na vivinjari vilivyopunguzwa uwezo wake, lakini simu nyingi za kisasa zina vivinjari kamili vinavyoweza kushughulikia teknolojia mpya za mtandao kama CSS 3, JavaScript, na Ajax.

Tovuti zilizobuniwa kufanya kazi vizuri kwenye vivinjari vya simu zinajulikana kama “mtandao wa simu.” Kwa sasa, zaidi ya 75% ya tovuti zinajulikana kuwa rafiki kwa simu kwa kutambua maombi yanayotoka kwenye vifaa vya mkononi na kuunda toleo linalofaa skrini ya kifaa hicho na kiolesura cha kugusa.

Remove ads

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads