Konde
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Konde ni jina la kihistoria kwa ajili ya Unyakyusa katika wilaya ya Rungwe nchini Tanzania na pia sehemu ya kaskazini ya Malawi kando la Ziwa Nyassa ambako umbo la jina ni "ngonde". Wenyeji wake waliitwa Wakonde tofauti na Makonde au Wamakonde wa Mkoa wa Mtwara.
Jina linaendelea kutumiwa hasa kwa ajili ya Dayosisi ya Konde ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania.
Kiasili maana ya kienyeji ya "Konde" ni tambarare na inamaanisha nchi tambarare kando ya Ziwa Nyassa upande wa kaskazini hadi milima ya Livingstone. Baadaye jina lilitumiwa pia kwa ajili ya maeneo yaliyokaliwa na Wakonde walioendelea kujenga vijiji kwenye mtelemko wa milima ya Rungwe na Uporoto inayopanda juu ya ncha ya kaskazini ya ziwa hilo.
Wakoloni Wajerumani waliitwa wakazi wote wa eneo hili "Konde" wakihesabu Wanyakyusa kama kundi kubwa kati yao.
Wakati wa utawala wa Waingereza jina la Unyakyusa lilianza kuwa kawaida kwa eneo lote upande wa Tanganyika.
Remove ads
Tazama pia
- Kwa kata katika wilaya ya Morogoro Vijijini inayoitwa vile tazama Konde (Morogoro)
- Kwa kata katika wilaya ya Micheweni inayoitwa vile tazama Konde (Pemba)
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads