Kuzimu

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kuzimu

Kuzimu ni huko ambako binadamu wanasadikiwa kuendelea kuishi baada ya kufariki dunia.

Thumb
Yggdrasil, mchoro unaojaribu kuonyesha imani ya watu wa Norwe kuhusu ahera kabla ya Ukristo kuenea nchini.
Thumb
Miguu ya mungu Vishnu wakati Kiumbe wa Kilimwengu akichora dunia na falme saba za Patala. Miguu inakalia nyoka Shesha.

Imani hiyo ni ya zamani sana na kujitokeza katika visasili na dini nyingi, kuanzia dini za jadi.

Ingawa imani hiyo ina tofauti nyingi, kwa jumla wengi wanasadiki mtu (au roho yake) anaendelea kuishi kama mzimu.

Katika Biblia kuna maendeleo ya ufunuo hata kuhusu suala la kuzimu, na ukamilifu wake uliletwa na Yesu ambaye alifundisha ufufuko wa wafu na uzima wa milele, lakini pia anasadikiwa kuwa kisha kufa alishukia kuzimu ili kutoa huko waadilifu wa kale kwa kuwatenganisha moja kwa moja na waovu na kuwaleta pamoja naye mbinguni.

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.