Lamine N'Diaye
Mwanasoka na kocha wa Senegal From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Lamine N'Diaye (alizaliwa Thiès, Oktoba 18, 1956) ni mwanasoka kutoka nchini Senegal ambaye kwa sasa ni Kocha wa Klabu ya TP Mazembe.
Uchezaji Mpira
N'Diaye alicheza nafasi ya kiungo. Alizitumikia timu za US Rail, SC Orange, Cannes na Mulhouse, alicheza pia timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Senegal.[1]
Ukocha
Mwaka 1998, N'Diaye aliifundisha klabu ya Mulhouse kwa muda mfupi.[2] Baadaye alihama na kufundisha klabu ya Coton Sport kuanzia mwaka 2003 mpaka 2006.[3] Mnamo January 2008, alikabidhiwa kikosi cha timu ya taifa ya Senegal, hii ni baada ya Henryk Kasperckzak kujiuzulu.[4] Mwaka huohuo mnamo Oktoba, alifutwa kazi ya kufundika timu ya Taifa.[5] Ilipofika Disemba 2008, N'Diaye aliteuliwa kuwa Meneja wa klabu ya nchini Moroko Maghreb Fez, na mwaka 2010 mwezi September, alipata kazi ya kufundika klabu ya TP Mazembe.[3] Mnamo Mei 2013, alibadili nafasi na kuwa mkurugenzi wa ufundi wa TP Mazembe.[6] Alipoondoka Mazembe 2014, alijiunga na AC Léopards kama Mkurugenzi wa Ufundi.[7] Ilipofika Julai 2018, akachukua nafasi ya Meneja kwenye klabu ya Al-Hilal.[8] Kazi ya kukinoa kikosi cha HoroyaAC alianza Novemba 2019.[9]
Remove ads
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads