TP Mazembe
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Tout Puissant Mazembe, maarufu kwa jina la TP Mazembe, ni klabu ya mpira wa miguu kutokea jiji la Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo.[1]
Historia
Tout Puissant Mazembe, ikiwa na thamani ya angalau milioni $10, ilianzishwa na watawa Wabenedikto waliokua wakisimamia shule ya Mtakatifu Boniface iliyopo Élisabethville (sasa Lubumbashi) katika jimbo la Katanga.[2] Mnamo mwaka 1939, wamisionari hao waliamua kuanzisha timu ya mpira wa miguu kwa ajili ya vijana wa shule waliokuwa wanashiriki skauti, mwanzoni, klabu hiyo ilipewa jina la Saint Georges FC, ikiwa ni njia ya kumuenzi kiongozi wa kikundi chao cha skauti. Klabu hiyo ilishiriki katika mashindano ya daraja la kwanza chini ya chama cha wachezaji wenyeji (FRASI) iliyoundwa na mfalme wa Ubelgiji. Ulipofika mwisho wa msimu, Georges walishika nafasi ya tatu.
Mnamo mwaka 1944, klabu hiyo ilianza kuonyesha mafanikio, na baadaye walibadilisha jina na kuitwa Saint Paul F.C., walipoamua kuchanganya wageni kwenye kuendesha timu, wamisionari waanzilishi waliamua kuachana na masuala ya usimamzi wa timu hiyo. Klabu ikaamua kubadili jina tena na kutumia jina la F.C. Englebertjina lililoakisi wazamini wakuu. Mwanzo wa jina la sasa"Tout Puissant" lilipatikana mwaka 1966, hii ni baada ya kushinda taji na kumaliza msimu huo bila kupoteza mchezo hata mmojawa.[1]
Mwaka 1960, Mazembe walibadilisha mfumo wa uongozi, hi ni mara baada ya DRC kupata uhuru mnamo 30 Juni 1960. Mwaka 1966, walishinda mataji matatu ya ndani, mataji hayo ni pamoja na National Championship, Coupe du Congo na Kombe la Katanga.
Miaka ya 1967 na 1968, walishinda mfululizo taji la African Cup of Champions. Walifanikiwa kufika hatua ya fainali mara nne mfululizo kuanzia mwaka 1967 mpaka 1970. Mazembe ndio timu ya kwanza Barani Afrika kushinda mfululizo taji la African Champions Cup. Mafanikio hayo yalikuja kujirudia kwa klabu ya Enyimba F.C mwaka 2003 na 2004.
Mazembe walipoteza ubora wao kwa takribani miaka 18. Shukrani ziende kwa Moïse Katumbi Chapwe gavana na mmiliki wa sasa wa klabu hiyo, kwani baada ya umiliki wake, Mazembe waliweza kuwa na kiwango bora cha ushindani katika soka la Afrika.
Mnamo Novemba 2009, Mazembe walifanikiwa kuchukua taji la Ligi ya vilabu bingwa Afrika. Walishinda dhidi ya Heartland F.C kwa kutoka sare ya 2–2, walishinda kwa ujumla wa magoli, sheria ya goli la ugenini.[3]
Kwa kushinda kwao taji hilo, Mazembe walifuzu kushiriki mashindano ya Kombe la Vilabu duniani vya mwaka 2009 chini ya FIFA. Licha ya kuongoza kwa goli moja kipindi cha kwanza, walipoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Pohang Steelers kutoka Korea Kusini kwa kufungwa magoli 2–1.[4]. Mchezo uliofuata walipoteza kwa kufungwa 3–2 dhidi ya Auckland City FC. Walimaliza mashindano wakiwa nafasi ya 6.[5][6]

Mwaka 2010, walishinda taji la Klabu Bingwa Afrika kwa mara nyingine tena, Ilipofika Disemba, waliweza kuweka rekodi kwa kuwa klabu ya kwanza Afrika kufika hatua ya fainali kwenye mashindano ya Kombe la Vilabu duniani. Walifika hatua hiyo kwa kuzifunga timu za C.F. Pachuca ya Meksiko 1–0 hatua ya Robo Fainali na Sport Club ya Brazili 2–0 hatua ya nusu fainali.[7][8] Walipoteza hatua ya Fainali iliyochezwa Disemba 18 kwa kufungwa goli 3 – 0 dhidi ya Inter Milan ya Italia.[9]
TP Mazembe walishinda taji lao la tano la Klabu Bingwa Afrika mwaka 2015, Walishinda kwa matokeo ya Jumla 4 – 1 dhidi ya USM Alger kutoka nchini Algeria.[10]
Remove ads
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads