Luxemburg
nchi katika Ulaya Magharibi From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Luxemburg (pia lusembagi ),rasmi kama Utemi Mkuu wa Luxemburg, ni nchi ndogo katika Ulaya ya Magharibi, inayopakana na Ubelgiji kaskazini na magharibi, Ufaransa kusini, na Ujerumani mashariki. Ina idadi ya watu takriban 672,050[1], ikiwa ya 167 duniani. Jiji lake kubwa zaidi ni Luxemburg, ambalo pia ni mji mkuu. Luxemburg imegawanyika katika majimbo 3—Diekirch, Grevenmacher, na Luxemburg. Inajulikana kwa kuwa moja ya nchi tajiri zaidi duniani,

Remove ads
Historia
Luxemburg kama nchi ndogo ilikuwa mara nyingi chini ya athira ya majirani wakubwa waliotawala juu yake kwa vipindi mbalimbali.
Kwa vipindi vingi vya historia yake Luxemburg ilikuwa sehemu ya Ujerumani.
Katika karne ya 14 watemi wa Luxemburg walichaguliwa kuwa wafalme wa Ujerumani.
Baada ya vita za Napoleoni, Ufaransa na Prussia zilivutana juu ya Luxemburg. Walipatana kwenye Mkutano wa Vienna (1815) ya kurudisha Luxemburg kama nchi ya pekee itakayotawaliwa na Mtemi Mkubwa. Mfalme wa Uholanzi alikuwa mtemi wa Luxemburg na nchi yenyewe iliungwa katika Shirikisho la Ujerumani.
Baada ya mwisho wa Shirikisho la Ujerumani (1866) Luxemburg haikujiunga (1870) na Dola jipya la Ujerumani.
Badiliko la familia ya kifalme katika Uholanzi lilisababisha uchaguzi wa mtemi wa pekee (1890).
Remove ads
Demografia
Ina wakazi 613,894 (Januari 2019) katika eneo la km² 2,586 pekee.
Kabila
Kati yao 49.1% ni wahamiaji kutoka Ureno (18.2% za wakazi wote), Ufaransa (13.5%), Ujerumani (10.3%), Italia (3.4%), Ubelgiji (3.3%), na nchi nyingine.
Lugha
Lugha ya taifa ni Kiluxemburg ambayo ni lahaja ya Kijerumani yenye athira nyingi za Kifaransa. Karibu wakazi wote huweza kuongea lugha hizo zote tatu na Kiingereza, lakini zaidi Kifaransa.
Dini
Upande wa dini, 68.7% wanajitambulisha kama Wakatoliki na 3.7% wanajitambulisha kama Wakristo wa madhehebu mengine. Waislamu ni 2.3%. Wasio na dini ni 26.8%.
Remove ads
Tazama pia
Marejeo
- Kreins, Jean-Marie (2003). Histoire du Luxembourg (kwa French) (tol. la 3rd). Paris: Presses Universitaires de France. ISBN 978-2-13-053852-3.
{{cite book}}
: CS1 maint: unrecognized language (link) - Thewes, Guy (Julai 2003). Les gouvernements du Grand-Duché de Luxembourg depuis 1848 (PDF) (kwa French) (tol. la Édition limitée). Luxembourg City: Service Information et Presse. ISBN 2-87999-118-8. Iliwekwa mnamo 10 Julai 2007.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link)
Remove ads
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads