Lava
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kwa matumizi mengine ya jina hili angalia lava (volkeno)

Lava (kutoka neno la Kiingereza larva ambalo lina asili ya Kilatini; pia bombwe) ni mtoto wa mdudu au wa mmojawapo wa invertebrata, amfibia au samaki katika hatua za awali za ukuaji wake.
Lava wa wadudu kadhaa wana majina ya pekee:
- jana ni lava wa nyuki
- buu na funza ni lava wa nzi na mbawakawa fulani
- kiluwiluwi ni lava wa mbu
- kiwavi ni lava wa kipepeo
- tunutu ni lava wa nzige
Kuna pia amfibia wanaopita hali ya lava. [[Ndubwi au kiluwiluwi ni lava wa chura.
Lava wa spishi mbalimbali huendelea kupitia hali ya pupa kabla ya kuendelea katika ngazi ya mwisho wa mabadiliko ya maumbile metafofosi.
Remove ads
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads