Lords of the Underground
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Akina Lords of the Underground (L.O.T.U.G.) ni kundi la muziki wa hip hop kutoka mjini Newark, New Jersey nchini Marekani. Kundi linaunganishwa na ma-MC watatu ambao ni Mr. Funke na DoItAll Dupré ambaye alikutana na DJ Lord Jazz (mwenyeji wa Cleveland) wote watatu walikutana wakati wanasoma katika Chuo Kikuu cha Shaw.
Kundi lilitoa albamu yao ya kwanza iliyoitwa jina la Here Come the Lords mnamo tar. 27 Septemba, 1993 huku suala la utayarishaji likishughulikiwa na Marley Marl na K-Def. Albamu ilishika nafasi ya 66 kwenye chati za Billboard 200 na imeingiza vibao vitano katika chati kadhaa nchini humo, ikiwa ni pamoja na kibao chao maarufu cha "Chief Rocka".
Kundi likaendelea kutoa albamu yao ya pili iliyoenda kwa jina la Keepers of the Funk kwa mwaka uliofuatia mnamo tar. 1 Novemba 1, 1994. Keepers of the Funk imefika kilele cha 47 kwenye chati za Billboard 200 na kuingiza vibao vikali vitatu katika chati kadhaa, kibao kilichotamba zaidi ni kile cha "Tic Toc". Kundi lilikufa mwaka wa 1995.
Mwaka wa 1999, kundi lilirudi tena uwanjani kwa kutoa albamu yao ya tatu iliyokwenda kwa jina la Resurrection. Ilitolewa kupitia studio ya Queen Latifah "Jersey Kidz", ilitolewa katika hali ya chini sana kiasi hata watu wengi wasijue kama albamu imetolewa. Mabwana walirudi tena mwaka wa 2007 kwa ajili ya albamu yao ya nne iliyoitwa House of Lords, lakini imekuwa kama ile ya Resurrection, imeanguka katika kufikia chati za Billboard.
Remove ads
Diskografia
Albamu za Studio
Singles
Remove ads
Viungo vya Nje
- Official website Ilihifadhiwa 26 Februari 2012 kwenye Wayback Machine.
- DJ Lord Jazz artist profile Ilihifadhiwa 7 Februari 2012 kwenye Wayback Machine.
- DJ Lord Jazz at MySpace
- LOTUG interview at britishhiphop.co.uk
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads