Kinyala

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Kinyala ni kata ya Wilaya ya Rungwe katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania. Msimbo wa posta ni 53535.

Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 13,632 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 12,871 [2] walioishi humo.

Kinyala inakaliwa na makabila makubwa mawili ambayo ni Wanyakyusa na Wasafwa.

Kata ya Kinyala ina shule 13 za msingi ambazo ni Igogwe, Lukata, Kakala, Isumba, Igembe, Kipande, Songwe, Ikukisya, Kisoko, Swaya, Isebelo, Malangali na Ishinga. Kuna pia shule za sekondari 3 ambazo ni Kinyala na Ziwa Ngosi ambazo ni za serikali na sekondari ya binafsi ya Lubala.

Kwa upande wa afya pia kuna hospitali kubwa moja ya Igogwe Hospital inayomilikiwa na Kanisa Katoliki, parokia ya Igogwe.

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads