Mababu wa Kitume
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mababu wa Kitume walikuwa Wakristo waandishi wa karne ya 1 na ya 2 BK ambao wanashika nafasi ya pekee kati ya Mababu wa Kanisa kutokana na ujirani wao na Mitume wa Yesu, ambao baadhi yao waliweza kuwafahamu au walau waliathiriwa nao sana kupitia mtu aliyewafahamu [1]. Ingawa baadhi ya maandishi yao yalitungwa wakati uleule wa vitabu kadhaa vya Agano Jipya na pengine yalitumika sana katika Kanisa la mwanzoni, hatimaye hayakupokewa katika Biblia ya Kikristo [2].
Remove ads
Maandishi yao
- Barua zinazohusiana na Papa Klementi I
- Barua ya kwanza ya Klementi
- Barua ya pili ya Klementi (wengi wanaona si ya kwake)
- Barua saba za Ignas wa Antiokia
- Kifodini cha Ignas
- Barua ya Polikarpo
- Kifodini cha Polikarpo
- Mabaki ya maandishi ya Papia wa Hierapoli
- Sehemu ndogo iliyobaki ya Apolojia ya Kwadrato wa Athens
- Didake
- Barua ya Barnaba
- Barua kwa Diogneto[3]
- Mchungaji, kazi ya Herma
Baadhi wanakubali pia Tenzi za Solomoni kama maandishi ya mwanafunzi wa Mtume Yohane ya katikati ya karne ya 1.[4]
Remove ads
Matoleo ya kitaalamu
- The Apostolic Fathers. Vol. 1. I Clement. II Clement. Ignatius. Polycarp. Didache. Barnabas. Loeb Classical Library. Cambridge: Harvard University Press, 1912 Kirsopp Lake
- The Apostolic Fathers. Vol. 2. Shepherd of Hermas. Martyrdom of Polycarp. Epistle to Diognetus. Loeb Classical Library. Cambridge: Harvard University Press, 1913 Kirsopp Lake
- The Apostolic Fathers. Vol. 1. I Clement. II Clement. Ignatius. Polycarp. Didache. Loeb Classical Library. Cambridge: Harvard University Press, 2003 Bart Ehrman (replaced Lake)
- The Apostolic Fathers. Vol. 2. Epistle of Barnabas. Papias and Quadratus. Epistle to Diognetus. The Shepherd of Hermas. Loeb Classical Library. Cambridge: Harvard University Press, 2005 Bart Ehrman (replaced Lake)
- The Apostolic Fathers: Greek Texts and English Translations. 3rd Edition. Grand Rapids: Baker, 2007 Michael Holmes
- Die Apostolischen Väter. Tübingen: Mohr Siebeck, 1992 Andreas Lindemann and Henning Paulsen (German)
Remove ads
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads