Bukoba (mji)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Bukoba ni manisipaa katika nchi ya Tanzania ambayo ni makao makuu ya Mkoa wa Kagera yenye postikodi namba 35100.
Bukoba iko kando ya Ziwa Viktoria Nyanza upande wa magharibi. Eneo lake liko chini ya Halmashauri ya Bukoba mjini (Bukoba Municipal Council) yenye madaraka ya wilaya.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa kuwa 144,938. Kulingana na sensa ya mwaka 2012 idadi ya wakazi wake ilihesabiwa kuwa 128,796[1].
Remove ads
Historia
Mji ulianzishwa mwaka 1890 wakati Wajerumani walipoteua sehemu hiyo kwa boma la jeshi lao la kikoloni. Likaendelea kuwa makao makuu ya mwakilishi mkazi Mjerumani katika falme ndogo za Karagwe, Washubi na Wahaya ambazo kwanza hazikuingizwa moja kwa moja katika koloni la Afrika ya Mashariki ya Kijerumani.
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads