Margerita wa Youville
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Margerita wa Youville (kwa Kifaransa Marie-Marguerite Dufrost de Lajemmerais d'Youville; Varennes, Quebec, 15 Oktoba 1701 – Montreal, Quebec, 23 Desemba 1771) alikuwa mwanamke Mkristo wa Kanada ambaye, baada ya kufiwa mumewe, alielekeza wanae wawili kwenye upadri akajitosa kwa nguvu zake zote kuhudumia wagonjwa, wazee na wenye shida za kila aina, akaanzisha shirika la kitawa la Masista wa Upendo wa Montreal [1].

Papa Yohane XXIII alimtangaza mwenye heri mwaka 1959, na Papa Yohane Paulo II mtakatifu tarehe 9 Desemba 1990, akiwa wa kwanza mzaliwa wa Kanada[2].
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[3] au 16 Oktoba.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads