Mbosso
Mwimbaji na mtunzi wa nyimbo wa Tanzania From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mbosso (anajulikana kwa jina la kisanii kama Mbwana Yusuph Kilungi; amezaliwa 3 Oktoba 1991) ni mwimbaji, mtunzi na mwanamuziki kutoka nchini Tanzania.
Umaarufu ulianza akiwa na kundi la Yamoto Band ambalo ndani yake kuliwa na Aslay, Beka Flavour, Enock Bella na Mbosso. Kwa pamoja walikuwa wanaunda Yamoto Band chini ya Mkubwa Fella na Wanawe. Jina la Mkubwa na Wanawe lilikuwa na hadi sasa bado lipo hivyo hivyo kama Mkubwa na Wanawe. Ndani ya mkubwa na Wanawe kuna vipaji mbalimbali.
Baada ya Yamoto Band kufa, Mbosso aliamua kurudi nyumbani kwao kijijini huko Kibiti. Ambapo alijihusisha na shughuli mbalimbali za kijamii ili kuyaendeleza maisha yake pia ilikuwa nafasi ya pekee mbosso kujipanga kurudi kwenye gemu la mziki wa bongo fleva. Jambo hili, lilikuwa tofauti kidogo na kina Aslay na Beka Flavour. Hawa waliendelea kutamba katika muziki hadi hapo Diamond Platnumz alipoona muda huu unafaa sasa kumrudisha Mbosso katika tasnia ya muziki kama alivyomuahidi mnamo mwakwa 2014 ya kwamba atamsaidia na kumuweka kwenye ramani ya muziki wa Bongo Flava. Wimbo wa kwanza wa Mbosso ulitoka mnamo tarehe 28 Januari 2018 na ulikwenda kwa jina la Watakubali.[1]
29 Januari alitambulishwa mbele ya hadhira ya kwamba yeye ni msanii kamili aliyesaini mkataba na WCB.[2]
Hadi sasa Mbosso ametoa wimbo kama vile Watakubali, Nimekuzoea, Alele, Shida, Picha Yake, Hodari, Nipepe, Hodari, Tamu. Kwa mwaka huu ametoa nyimbo kama tunapendana akiwa ameshirikiana na "D Voice". Wimbo mwingine aliotoa na kundi la Wasafi jina lake lilikuwa Zilipendwa na wimbo mwingine aliotoa na Diamond Platnumz na Lavalava wimbo ambao jina lake ni Jibebe. Pia msanii Mbosso ana matatizo ya ki afya yanayo mkabili rejea maneno yake yanasema ninaugonjwa wa kutetemeka.
Mbosso, msanii wa Bongo Flava kutoka Tanzania, ametoa nyimbo nyingi zilizopendwa na mashabiki. Mnamo Machi 2021, alitoa albamu yake ya kwanza iitwayo Definition of Love, yenye nyimbo 12 na ushirikiano na wasanii mbalimbali.
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads