Meridian Bet Tanzania
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Meridian Bet Tanzania ni waendeshaji wa michezo ya kubahatisha nchini Tanzania. Kampuni hiyo ina leseni ya kuendesha michezo ya bahati nasibu katika sekta zote za ubashiri, ikiwa ni pamoja na maduka ya kubashiri[1] na ubashiri wa mtandaoni[2]. Mpaka sasa, Meridian Bet inaendesha shughuli zake katika mikoa yote Tanzania.[3]
Remove ads
Historia
Meridian Bet Tanzania ilianzishwa mwezi Juni mwaka 2017. Taasisi hii inamilikiwa na kampuni ya Bit Tech Limited, kampuni yenye leseni ya kufanya kazi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa usajili wa namba 135726 kutoka kwa Mamlaka ya Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania. Kwa sasa kampuni ya Meridian Bet Tanzania inaendesha biashara zake katika miji takribani yote nchini Tanzania.
Mfumo wa biashara
Biashara kubwa ya Meridianbet Tanzania ni ya kuendesha biashara ya Kubashiri Michezo, lakini pia Kasino ya Mtandaoni na Sloti. Imepewa leseni kwa ajili ya Kubashiri kwa Njia ya Ujumbe Mfupi USSD Ilihifadhiwa 11 Septemba 2021 kwenye Wayback Machine. kutoka kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).[4]
Washirika
Meridian Bet Tanzania ina washirika wengi wa kimataifa, ikiwa ni pamoja na Meridian Gaming ambao hufanya usambazaji wa programu za kubashiri michezo na kasino za mtandaoni kwenye maduka yake na vilevile kwenye mitandao.[5]
Bidhaa na Huduma
Meridian Bet Tanzania inafanya kazi katika maduka 100 ya kubetisha na vile vile katika tovuti yake ya mtandaoni. Lengo kuu la kampuni hii ni kujikita katika Kubashiri Michezo (kabla ya mechi kuanza na pale zinapokuwa zimeanza) na vile vile kutoa huduma zingine kama vile kasino na odds za mechi kadha wa kadha.[6]
Ubashiri wa Mtandaoni
Licha ya kuendesha michezo ya kubashiri kwa mtandao, Meridian Bet Tanzania pia inaendesha michezo ya kasino ya mtandaoni na aina zingine za michezo ya kubashiri
===Huduma Katika Maeneo Maalumu=== Meridianbet ina mfumo kamilifu wa suluhisho la ubashiri katika maeneo maalumu ya maduka. Hii inafanya kazi kama eneo lililoandaliwa maalumu kwa ajili ya ubashiri salama katika maduka, huku kukiwa na mfumo salama wa uendeshaji, uongozi, ripoti na masuala ya kodi.
Remove ads
Programu ya Apple Watch
Meridian Bet ni waendeshaji wa michezo ya kubashiri wa kwanza kuwapa wateja wake huduma ya programu ya Apple Watch. Programu hii inawasaidia watumiaji kufahamu matokeo moja kwa moja, na kupata taarifa na kufurahia ubashiri moja kwa moja. Apple Watch imeunganishwa moja kwa moja na mfumo wa kampuni wa iOS.
Sera za Ubashiri
Meridian Bet Tanzania ina sera makini za kubashiri kistaarabu ambazo zinatokana na misimamo tajwa hapa chini;
- Kulinda dhidi ya uraibu wa michezo ya kubashiri
- Kulinda watoto dhidi ya shughuli za ubashiri
- Usalama wa wachezaji na makundi maalumu
- Usalama wa mchezo
Huduma kwa Jamii
Kama Kampuni, Meridianbet Tanzania inaamini katika kusaidia na kuinua makundi mabalimbali nchini yenye uhitaji, na wamekuwa wakifanya hivyo. Katika kipindi cha janga la Virusi vya Corona, Meridianbet iliendelea kushirikiana jamii na kutoa faraja wa makundi maalumu.
Meridianbet Tazania imekuwa ikitoa misaada kwa kaya za vijijini[7], wagonjwa mabilimbali[8], hostpitali[9][10], waathirika wa madawa ya kulevya na makundi mengine muhimu[11][12]. Kampuni pia imekuwa ikiwasaidia wafanyakazi wake katika kuboresha maisha yao na maisha ya familia zao.
Remove ads
Ukuaji Kimataifa
Meridianbet imekuwa na rekodi nzuri ya kujitanua zaidi kuyafikia maeneo mapya moja kwa moja au kwa uwakilishi kupitia mfumo wake wa biashara. Meridianbet inatazama fursa za kufanya kazi na nchi zenye uthibiti na pale ambapo fursa za kutokuwepo udhibiti zinatokea.
Soma pia
Tanbihi
Kiungo cha nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads