Meroë
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Meroë (kwa Kimeroe: Medewi au Bedewi) ni jina la mji wa kale. Mabaki ya majengo yake yanapatikana kwenye ukingo wa mashariki wa mto Nile karibu kilomita 6 kaskazini mashariki mwa Kabushiya karibu na Shendi, nchini Sudan. Meroe iko mnamo kilomita 200 kaskazini mashariki mwa Khartoum kando ya barabara kuu kutoka Khartoum kuelekea Atbara. Karibu kuna vijiji vichache ambavyo vinaitwa Bagrawiyah.
Meroë ilikuwa mji mkuu wa Ufalme wa Kushi kwa karne kadhaa. [1]
Remove ads
Urithi wa Dunia

Tangu Juni 2011 eneo la Meroe limeandikishwa katika orodha ya UNESCO inayotaja "Urithi wa Dunia.[2]
Meroe inajulikana kwa piramidi zake nyingi. Piramidi hizo si kubwa kama zile za Gizah katika Misri lakini idadi ni kubwa, kwa jumla zilikuwa zaidi ya 200.
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads