Metarhizium acridum

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Metarhizium acridum[1] ni jina jipya la kundi la matenganisho ya kuvu ambayo yanajuliwa kusababisha maambukizi dhidi ya spishi za Acrididea pekee. Zamani spishi hii ilikuwa na hadhi ya namna katika Metarhizium anisopliae (var. acridum[2]). Kabla ya hii matenganisho haya yalitambulishwa kama M. flavoviride au Metarhizium sp.[3] Yaunda kundi la matenganisho kutoka panzi na nzige ambayo yanafanana sana.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi ...
Remove ads

Biolojia

M. acridum inaambukiza takriban pekee panzi wa nusuoda Caelifera ya Orthoptera. Makundi kadhaa ya uchunguzi, k.m. mradi wa mataifa LUBILOSA, ambao umeendeleza dawa ya kibiolojia “Green Muscle”, yametambua na yameshughulikia changamoto za kifundi za matumizi ya udhibiti wa visumbufu kwa vijidudu, kujumuisha: uchaguzi wa matenganisho, uzalishaji kwa wingi na njia za matumizi (michanganyiko na mapulizaji).[4] Kwa maneno mengine udhibiti wa wadudu unaegemea vipengele kama namba ya spora ipulizwayo juu ya wadudu, mchanganyiko[5] na hali ya hewa.[6] Michanganyiko katika mafuta inawezesha upulizaji wa spora za kuvu wakati wa hali kavu na inafalia upulizaji kwa mashine za kiwango kidogo sana zinazotumika kwa udhibiti wa nzige.

M. acridum inaambukiza panzi na nzige tu. Wanasayansi walitaka kujua kwa nini kimelea hiki ni mahususi kwa shabaha yake. Wanafikiri kwamba sababu ni ukosa wa jeni Mest1 katika M. acridum. Utafiti wa wanasayansi wa Uchina ulijaribu shughuli ya jeni hii. Walikuwa wakitumia aina ya M. robertsi isiyo na jeni Mest1 ifanyayo kazi, wanasayansi waliona kwamba kuvu hii iliweza kuambukiza panzi na nzige tu kama M. acridum kabisa.[7]

Sasa USDA inafikiria kuhusu uachiaji wa M. acridum katika MMA ya magharibi ili kudhibiti panzi na nyenje wa kienyeji.[8]

Remove ads

Matenganisho maalum

  • IMI 330189 (= ARSEF 7486) ni mfano wa zamani wa spishi na ilipatwa huko Niger: kiambato cha utendaji cha “Green Muscle”.
  • CSIRO FI 485 (= ARSEF 324) ni tenganisho la Australia: kiambato cha utendaji cha “Green Guard”.

Marejeo

Tazama pia

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads